RABAT-Timu ya Morocco imefanikiwa kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026 baada ya kuifunga Taifa Stars mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa nchini humo.
Ni katika mtanange uliopigwa usiku wa kuamkia Machi 26,2025 katika dimba la Honor mjini Oujda, Morocco.
Mabao ya Morocco katika Kundi E yamefungwa na Nayef Aguerd dakika ya 51′ huku Brahim Abdelkader Díaz akifunga kwa mkwaju wa penalti bao la pili dakika ya 58′.
Kwa matokeo hayo, Morocco imekuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Aidha, katika kundi hilo lenye timu sita vinara ni Morocco wakiongoza alama 15, Niger alama sita,Tanzania alama 6,Zambia alama tatu,Eritrea ambao hawana alama hata moja na Congo alama sufuri.