KOCHA Mkuu wa Yanga, Hamdi Miloud ameweka wazi wachezaji wake wanafanya kazi kubwa kutafuta matokeo uwanjani jambo ambalo linapaswa kuwa endelevu kutokana na ushindani uliopo ndani ya ligi.
Ipo wazi kwamba ndani ya Februari kocha huyo ametwaa tuzo ya kocha bora baada ya kuwashinda wawili aliongia nao kwenye fainali ya kumtafuta kocha bora.
Katika mechi hizo tano safu ya ushambuliaji ya Yanga ilifunga mabao 16 na ukuta uliruhusu mabao mawili pekee kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Ni Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Yanga na Fred Minziro Kocha Mkuu wa Pamba hawa aliingia nao fainali na kuwashinda kwenye kuwania tuzo hiyo na mchezaji alichaguliwa kuwa Prince Dube ambaye anapewa mbinu na kocha huyo.
Miloud amesema kila mchezo ambao wanacheza una ushindani mkubwa jambo ambalo linawafanya wapambene kupata matokeo mazuri kila wanapoingia uwanjani.
“Ushindani ni mkubwa na wachezaji wanajituma kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo nina amini kwamba tutaendelea kuwa kwenye ushindani katika mechi zinazofuata.”
Yanga ni vinara kwenye ligi wakiwa na pointi 58 baada ya mechi 22, safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayoongozwa na Dube na Clement Mzize wenye mabao 10 kila mmoja imetupia mabao 58.
Yanga imetinga hatua ya 16 bora kwenye CRDB Federation Cup kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex ilikuwa ni Machi 12 2025 mabao mawili yalifungwa na Maxi Nzengeli na bao moja likifungwa na Clement Mzize.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.