Beki kisiki wa klabu ya Yanga SC Ibrahim Hamad ‘Bacca’ amepandishwa cheo na Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) kutoka Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora kwenye mchezo wa soka.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Sajenti Ibrahim Bacca ambaye wazazi wake pia ni askari amesema “Sina budi kushukuru kikosi changu kwa kuweza kunisapoti kwa kila hatua. Nitaendelea kuipambania nchi yangu”
KMKM iliyomwachia Bacca kuitumikia Yanga, ni kikosi cha ulinzi cha Zanzibar ambacho kina jukumu la kulinda mipaka ya bahari dhidi ya magendo, uvuvi haramu, na vitendo vingine vya kihalifu.
Vilevile KMKM husaidia katika operesheni za uokoaji baharini na usalama wa majini.