YANGA ndani ya Uwanja wa Mkapa, Machi 8 2025 kwa ajili ya mchezo wa Kariakoo Dabi ambao umeahirishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB).
Licha ya taarifa kutolewa na TPLB kuhusu kuahirisha mchezo namba 184 kati ya Yanga na Simba ambao ni Kariakoo Dabi, wenyeji Yanga wamewasili Uwanja wa Mkapa.
Mapema Yanga kupitia kwa Mtendaji Mkuu, Andre Mtine ilitoa taarifa kwa Umma kuwa mchezo wao dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa saa 1:15 upo palepale na hakuna mabadiliko yoyote.
Yanga wameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo na kufika kwao Uwanja wa Mkapa inamaanisha kwamba wapo tayari kwa mchezo.
Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wamefika Uwanja wa Mkapa ni Aziz Ki, Clatous Chama, Israel Mwenda, Diarra, Bacca, Kennedy Musonda.
Taarifa kutoka TPLB imeeleza kuwa itatoa taarifa kuhusu tukio la Simba kutoa taarifa kwamba walizuiwa kufanya mazoezi kikanuni na kutangaza tarehe ya mchezo huo mapema iwezekanavyo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.