YANGA KAMILI KWA KARIAKOO DABI, KIPENGELE HAKUNA

MABOSI wa Yanga wamebainisha kuwa hakuna kipengele kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ambao unatarajiwa kuchezwa leo Machi 8 2025, saa 1:15 Uwanja wa Mkapa.

Uongozi wa Simba usiku wa kuamkia Machi 8 2025 walitoa taarifa kwamba hawatashiriki mchezo kutokana na kutopewa ruhusa ya kufanya mazoezi Uwanja wa Mkapa siku moja kabla ya mchezo.

Wakati hayo yakitokea Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara taarifa rasmi kupitia ukurasa wa Instagram imeeleza namna hii: “Ile siku imefika.” Taarifa hiyo imesindikizwa na ujumbe wa mechi ya Kariakoo Dabi ambayo inatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa.

Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba haupo tayari kwa mchezo wa leo na wamegomea mazima suala hilo kwa mujibu wa kanuni.

Iliwahi kutokea Mei 8 2021 ambapo uongozi wa Yanga uligomea mechi ya Dabi kwa kueleza kuwa mabadiliko ya muda yalifanyika kinyume na utaratibu kwa mujibu wa kanuni namba 15 ambayo ilikuwa inaeleza kuwa mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali.

Katika siku hiyo Yanga walipeleka timu muda wa awali saa 11:00 jioni badala ya saa 1:00 usiku muda ambao Simba walipeleka timu. Mwisho mchezo huo ulipangiwa siku nyingine ambapo Yanga ilipata ushindi kwa bao 1-0 lililofungwa na Zawad Mauya.

Taarifa zinaeleza kuwa Yanga wao wapo tayari kwa mchezo na watapeleka timu kama ilivyo kawaida na hawana kipengele isipokuwa Simba wao wamegomea.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.