TAMKO KUTOKA BODI YA LIGI SUALA LA KARIAKOO DABI

BAADA ya Simba kutoa taarifa kuwa wanagomea mechi kwa kuwa walizuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mkapa hivyo hawatacheza mchezo wa Machi 8 2025, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Steven Mguto amesema wanalifanyia kazi.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa leo ni mzunguko wa pili baada ya ule wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-1 Yanga unatarajiwa kuchezwa saa 1:15 usiku kwa wababe hawa kukutana uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.

Mguto amesema: “Najua huu mgogoro na sio kitu cha kupuuzwa hivyo tutafanyia kazi kwa naitisha kikao asubuhi cha saa 72 ndiyo kamati ambayo inafanyia kazi kwenye kuendesha ligi hivyo tutafanyia kazi na umma utajulishwa.

“Usiniulize ninafanyia kazi kitu gani mpelelezi huwezi kumwambia kazi yao unaifanyia namna gani, sisi tuna namna yetu, wasubiri ni kitu nyeti sio kitu cha kudharau wanaweza kuwa Simba wanahoja hivyo tutajua. Sisi wakati tunatengeneza kanuni na tukishazipitisha kila mdau anakuwa nazo kanuni.”

Chanzo: EFM

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.