KWA ARAJIGA WAKIPATA PENATI HAWA HAPA WATAZIPIGA

BADO siku mbili Kariakoo Dabi ichezwa Uwanja wa Mkapa Machi 8 2025 ambapo joto limezidi kupanda kwa kila pande kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ni Yanga ambao katika mzunguko wa kwanza walikomba pointi tatu mazima baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga hivyo mchezo wa mzunguko wa pili ni kivumbi na jasho.

Mwamuzi ametangazwa Ahmed Arajiga ambaye atakuwa kwenye majukumu yake kutimiza sheria 17 za soka hivyo ikiwa itatokea akatafsri penati kwa timu yoyote ile ambayo itakuwa imechezewa faulo basi kuna mitambo ambayo itapewa kazi yakupiga penati.

Mapigo ya penati yamekuwa yakitolewa kwenye mechi nyingi Bongo kutokana na tafsri ya mwamuzi na rekodi zinaonyesha kuwa timu namba moja kupata penati nyingi ni Simba ambazo ni 10 na katika mchezo dhidi ya Namungo Simba ilipata penati tatu katika hizo mbili zilifungwa na moja iliokolewa.

Shukrani kwa Joathan Nahimana kipa wa Namungo ambaye aliokoa penati iliyopigwa na Leonel Ateba mshambuliaji chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Ikiwa katika mchezo wa Kariakoo Dabi, Yanga watapata penati kazi itapewa kwa Aziz Ki ambaye katika penati 7 ambazo walipata kwenye mechi za ligi huyu alipiga sita, alifunga nne akikosa penati mbili ndani ya uwanja.

Mwingine ni Pacome ambaye alifunga penati moja kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Kwa Simba ni Jean Ahoua na Leonel Ateba kati ya hawa watapewa kazi yakupiga penati ikitokea kwa kuwa wamekuwa wakifanya hivyo kwenye mechi za ligi.

Ahoua kapiga penati 5 zote akifunga na Ateba kapiga penati 5 akifunga nne na kukosa penati moja kwenye mchezo dhidi ya Namungo, Uwanja wa Majaliwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.