MSHINDI WA BSS NI MOSES LUKA, DIAMOND PLATNUMZ ATANGAZA KUWASAINI

SUPASTAA wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameweka wazi kuvutiwa na vipaji vya Mshindi wa kwanza na Wapili wa BSS ili kuwasaini katika Lebo yake hiyo.

Diamond ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Machi 1, 2025 katika fainali ya mashindano hayo ya kusaka vipaji ya Bongo Star Seach (BBS) Warehouse, Masaki jijini Dar es Salaam.

Mshiriki kutoka DRC, Moses Luka ameibuka Mshindi wa Shindano la 15 la kusaka vipaji (Bongo Star Search – BSS) msimu wa 2024/25 na kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni 20 na zawadi nyingine mbalimbali.

Moses Luka alieiwakilisha DRC amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitisha Mkutano wa pamoja wa EAC-SADC kuhusu amani ya mashariki mwa DRC.