KIPA WA SIMBA AMEWEKA UFALME WAKE

KIPA namba moja wa Simba, inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids amejenga ufalme wake kwa makipa ambao wana hati safi nyingi ndani ya ligi yeye ni kinara, Mousa Camara ambaye ni chaguo la kwanza ndani ya timu hiyo.

Kipa huyo ni mechi 18 kacheza akikomba dakika 1,620 akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliokomba dakika nyingi ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.

Camara kafungwa mabao sita ndani ya ligi namba nne kwa ubora ilikuwa mabao mawili dhidi ya Coastal Union, mawili dhidi ya Kagera Sugar, bao moja dhidi ya Yanga na bao moja dhidi ya Fountain Gate.

Kwenye Kariakoo Dabi Camara alionekana kufanya makosa katika kuokoa mpira wa faulo iliyopigwa na kiungo Clatous Chama uliporudi ndani ya uwanja ukakutana na Maxi Nzengeli ambaye alipiga krosi kuelekea langoni ikakutana na Kapombe Shomari ambaye aliokoa hatari hiyo.

Wakati Kapombe akimalizia kuokoa hatari beki wa Simba, Kelvin Kijili aliyekuwa karibu na lango la Simba mpira ule ukamgonga na kuzama mazima nyavuni, Simba ikayeyusha pointi tatu mazima.

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra amekaa langoni kwenye mechi 12 akikomba dakika 1,080 ni mabao matano kafungwa kipa huyo ndani ya msimu wa 2024/25 akiwa na hati safi 9.

Wakali hao wanatarajiwa kukutana ndani ya uwanja kwenye Kariakoo Dabi inayotarajiwa kuchezwa Machi 8 2025, Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.