CHAMA KWENYE MTIHANI YANGA, KAZI IPO

CLATOUS Chama ndani ya kikosi cha Yanga yupo kwenye mtihani wa kupambania namba kikosi cha kwanza kwa kuwa kwa sasa hajawa  chaguo la kwanza msimu wa 2024/25 baada ya kuibuka hapo akitokea kikosi cha Simba.

Ipo wazi kwamba alipokuwa ndani ya kikosi cha Simba Chama alikuwa ni chaguo la kwanza kwenye eneo la kiungo tofauti na sasa maisha yake ndani ya changamoto mpya Jangwani.

Katika mechi 18 ambazo Yanga imecheza ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Chama amecheza mechi 14 akikosekana kwenye mechi nne ambapo mechi nyingi ambazo alicheza alianzia benchi na zile ambazo alianza kikosi cha kwanza ilikuwa ngumu kukomba dakika 90.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita wa Yanga dhidi ya JKT Tanzania ugenini Chama alianza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi lakini hakukomba dakika zote 90 nafasi yake ilichukuliwa na Aziz Ki kipindi cha pili dakika ya 45.

Ni dakika 591 amekomba akitoa pasi mbili za mabao na kufunga bao moja kati ya mabao 42 yaliyofungwa na timu hiyo namba moja katika kufunga mabao mengi ikiwa na pointi 46.

Kituo kinachofuata kwa Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi ni Februari 14 2025 itakuwa dhidi ya KMC, Uwanja wa KMC Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.