Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kufikia makubaliano na klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco juu ya kuwauzia mshambuliaji Selemani Mwalimu kwa mkataba wa moja kwa moja kwa dau ambalo hawajaweka wazi (undisclosed fee).
Taarifa ya leo Januari 31, 2024 iliyotolewa na Singida Black Stars imebainisha kwamba sehemu ya makubaliano hayo ni klabu hiyo kunufaika na asilimia 10% ya mauzo ya baadae (sell-on) endapo Wydad AC itamuuza kwenda klabu nyingine.