MWAMBA mwenye kucheza na kutoa maelekezo ndani ya kikosi cha Yanga, Pacome Zouzoah ni pasua kichwa kutokana na uwezo wake kwenye kupiga pasi ndefu na fupi akiwa uwanjani.
Nyota huyo kwenye dirisha dogo ilikuwa inatajwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi wa Simba kwa kuwa mkataba wake unagota mwisho inaelezwa kuwa mabosi wa Yanga walifanya mazungumzo naye kuhusu kuboresha mkataba wake.
Hivi karibuni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally aliweka wazi kuwa wanamfuatilia mchezaji huyo kwa kuwa wanatambua mkataba wake unakaribia kuisha wakiona anafaa watahangaika naye.
“Kuna mchezaji ambaye yupo pale ambaye ni Pacome huyu tunamfuatilia tukiona anatufaa basi tutahangaika naye kwa kuwa tunajua kwamba mkataba wake unaisha.”
Pacome ndani ya ligi amecheza jumla ya mechi 14 kati ya 15 akikosekana kwenye mchezo mmoja akisepa na dakika 803 uwanjani akifunga mabao 5 na kutoa pasi tatu za mabao.
Yanga kwa sasa ipo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex, Februari Mosi 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.