MSAADA WA MASHUKA WATOLEWA ZAHANATI YA ALIMAUA

Kampuni ya Meridianbet, kwa mara nyingine tena, imeonyesha dhamira yake ya kusaidia jamii kupitia mchango mkubwa kwa Zahanati ya Alimaua ambapo safari hii  kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa mashuka kwa zahanati hiyo, kama sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za afya na mazingira ya kutolea huduma kwa wananchi wa eneo la Alimaua.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, kiongozi wa msafara huo Bi Nancy Ingram. Amesema kuwa msaada huo utaongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa hapo na pia wanajivunia kuchangia katika kuboresha maisha ya wananchi na kuhakikisha kuwa huduma za afya zinazotolewa zinakuwa bora zaidi. Hiyo ni sehemu ya dhamira yao ya kusaidia jamii, na watendelea kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za kijamii.

Vilevile Meridianbet inakuambia hivi bashiri mechi za Europa leo uweze kupiga pesa sasa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao. Jisajili hapa.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa msaada wa mashuka utasaidia katika maeneo mbalimbali ya zahanati, ikiwa ni pamoja na vyumba vya kulaza wagonjwa na maeneo ya kujifungulia, ambapo mahitaji ya vifaa kama hivyo ni muhimu. Kampuni ya Meridianbet imedhamiria kuendelea na mipango ya kusaidia jamii, hasa katika sekta za afya na elimu.

Kwa upande wake, Zahanati ya Alimaua kupitia mwakilishi wao walielezea shukrani zao kwa msaada huo na kusema, “Tunashukuru sana kwa msaada huu kutoka kwa Meridianbet. Mashuka haya yatasaidia sana katika kuboresha hali ya huduma kwa wagonjwa wetu. Huu ni msaada muhimu kwa zahanati yetu, na tunapenda kuonyesha shukrani zetu kwa kampuni hii kwa mchango wao mkubwa.”

Meridianbet inaendelea kuonyesha msaada wake kwa jamii kupitia michango kama hii, ambapo kampuni inasisitiza umuhimu wa kujali na kusaidia katika maeneo yanayohitaji msaada mkubwa. Kwa kufanya hivyo, Meridianbet inachangia katika kuboresha maisha ya watu na kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.