KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki anatajwa kuwa kwenye rada ya Klabu ya Wydad Casablanca ambayo inahitaji saini yake.
Ki msimu wa 2023/24 mezani alikuwa na ofa zaidi ya mbili kutokana na kiwango ambacho alionyesha akiwa Yanga na mwisho alisaini dili jipya kuendelea kuwa ndani ya Yanga.
Ikiwa Wydad Casablanca watakakuwa wanahitaji saini ya Ki lazima wawe tayari kuvunja akaunti ya benki kwa kutoa mkwanja mrefu kwa kuwa kiungo huyo bado ana mkataba na Yanga.
Rekodi zinaonyesha kuwa nyota huyo alitoa jumla ya pasi 8 za mabao alitupia mabao 21 kwenye mechi 27 kati ya 30 ndani ya kikosi cha Yanga zama za Miguel Gamondi.