KUNA mastaa ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids wakipewa majukumu ya kupiga penati asilimia 100 wamekuwa wakiwapa tabu makipa kwa kufunga kwenye mchezo husika iwe kitaifa ama kimataifa.
Simba kwenye penati ambazo wamepata kwa msimu wa 2024/25 ndani ya uwanja hakuna ambayo wamekosa miongoni mwa waliyofunga ni katika anga la kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ilikuwa dhidi ya Bravos na mpigaji alikuwa ni Jean Ahoua.
Ahoua ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Simba na Leonel Ateba mshambuliaji kiongozi ndani ya kikosi hicho ambacho ni namba moja kwenye msimamo kikiwa na pointi 40 wamekuwa wakipewa majukumu ya mapigo hayo huru.
Ahoa na Ateba wote ni wakali kwenye mapigo ya penalti ndani ya ligi wakati rekodi zikionyesha kuwa Simba walipata penalti sita ndani ya mzunguko wa kwanza na zote wamefunga, wafungaji ni Ateba na Ahoua kila mmoja akitupia mabao matatumatatu.
Kinara kwa kucheza na nyavu ndani ya Simba ni Ahoua mwenye mabao 7 ambapo mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia yote kafunga akitumia mguu huo ndani ya ligi na ametoa pasi tano za mabao.
Ahoua amehusika kwenye mabao 12 yaliyofungwa na Simba kati ya 31 ikiwa ni timu namba mbili kwenye orodha ya timu zenye mabao mengi huku Ateba akiwa katupia mabao matano ndani ya ligi.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mstari wa mbele wat imu hiyo unatisha kutokana na ubora walionao wachezaji kwenye kufunga na kutengeneza nafasi za mabao.
“Mstari wa mbele wa Simba unatisha vibaya mno, una Ateba, Ahoua, Mpanzu, Kibu Dennis hakika haw ani wachezaji wenye uwezo mkubwa vibaya mno wanaendeleza ubaya ubwela kwa wapinzani.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.