KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Sead Ramovic ujanja wake upo kwenye mguu wake wa kushoto ambao umekuwa na mashuti yenye nguvu kitaifa na kimataifa.
Ki anaingia kwenye rekodi ya nyota aliyepiga mashuti mengi katika mechi za hatua ya makundi huku mchezo dhidi ya Al Hilal ukitajwa kuwa ni mchezo aliocheza katika ubora wa hali ya juu ugenini.
Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mchezo dhidi ya Al Hilal Ki alipiga jumla ya mashuti matano ambayo yalilenga lango huku moja likiwa ni bao la mapema kabisa dakika ya 7 likiwapa pointi tatu Yanga ugenini.
Ikumbukwe kwamba Al Hilal mchezo wao kupoteza katika hatua ya makundi ilikuwa mbele ya Yanga iliyokuwa ugenini na mchezo wa pili ilipoteza dhidi ya TP Mazembe.
Ki kwenye Ligi Kuu Bara amefunga mabao mawili kama ilivyokuwa kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, ana kazi ya kutetea kiatu cha ufungaji bora ndani ya ligi namba nne kwa ubora.
Msimu wa 2023/24 Aziz Ki alifunga mabao 21 katika hayo alifunga hat trick mbili na alitoa pasi 8 za mabao kwenye mechi 27 ambazo alipata nafasi ya kucheza mchezaji bora wa msimu uliopita.
Msimu wa 2024/25 Ki amecheza mechi 15 akitoa pasi nne za mabao huku akifunga mabao mawili kwenye dakika 1,084 alizocheza huku ujanja wake ikiwa ni mguu wa kushoto ambapo kafunga mabao mawili na yote kwa mapigo ya penalti kumbuka kwamba alikosa penalty moja kwenye mchezo dhidi ya Tabora United.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.