KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kimemalizana na wapinzani wao Kilimanjaro Wonders kwa maajabu ya mtoto wa maajabu Chasambi kupachika bao huku David Kameta akitoa pasi mbili za mabao kwenye ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo wa CRDB Federation Cup.
Simba walianza kupata bao la mapema kwenye mchezo wa leo ikiwa ni dakika ya kwanza kupitia kwa mshambuliaji Valentino Mashaka akiwa ndani ya 18 katika sekundi ya 25 kwa mguu wake wa kulia.
Hiyo ilikuwa ni mwanzo kabisa wa mchezo na iliwachukua dakika tatu Simba kufunga bao la pili kupitia kwa kiungo wa maajabu Ladack Chasambi ilikuwa dakika ya nne muda mfupi baada ya Mashaka kuwaondoa mashaka mashabiki wa Simba.
Kabla hawajapoa Kilimanjaro Wonders walikutana na maajabu mengine dakika ya 9 katika harakati za kuokoa hatari ndani ya 18, nyota Patrick Sebastian alijifunga bao likiwa ni bao la tatu.
Joshua Mutale kiungo mshambuliaji wa Simba ambaye alianza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Fadlu Davids yeye alifunga bao la nne ilikuwa dakika ya 20 kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup na dakika zilizoongezwa kipindi cha pili zilikuwa ni tatu.
Dakika ya 45 ilibaki kidogo Kilimanjaro Wonders kuonyesha maajabu yao kwa kumtungua AllySalim baada ya nyota wa Okejapha kufanya makosa kwenye kuokoa hatari bahati ikawa kwa Salim kwa kuwa mpigaji alkosa utulivu mpira ukatoka nje ya lango.
David Kameta ambaye alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Kilimanjaro Woders alikuwa kwenye kutimiza majukumu yake alitoa pasi yake ya kwanza dakika ya nne ikakutana na Chasambi.
Kipindi cha pili Kameta alitoa pasi dakika ya 48 ikakutana na Steven Mukwala akaruka juu waaa na bao la sita likifungwa na Edwin Balua dakika ya 79 akitumia pasi ya Mutale.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.