MUTALE, DUCHU, MZAMIRU WAANZA KIKOSI CHA KWANZA

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba, Mzamiru Yassin ameanza kikosi cha kwanza dhidi ya Kilimanjaro Wonders ikiwa ni mchezo wa CRDB Federation Cup.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi, Yanga walishuka uwanjani Januari 25 2025 na kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Copco huku nyota Israel Mwenda ingizo jipya likianza kikosi cha kwanza na uzi wa Yanga.

Fadlu ameanza na kikosi cha namna hii mbele ya Kilimanjaro Wonders ambapo Kibu Dennis, Leonel Ateba na Camara hawa hawapo kabisa kwenye mpango kazi wa leo.

Kikosi cha kwanza ni: Ally Salim, David Kameta, Nouma, Chamou, Hamza Jr, Okejapha, Ladack Chasambi, Mzamiru Yassin ambaye ni nahodha, Valentino Mashaka, Awesu Awesu na Joshua Mutale.

Akiba ni Hussen Abel, Kelvin Kijili, Kazi, Kagoma, Omary, Mukwala, Debora,Balua na Alexander.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.