UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zilizopo mbele yao ikiwa ni pamoja na mchezo wa CRDB Federation Cup ambao dhidi ya Copco.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex Januari 25 2025 ikiwa ni mchezo wa mtoano na Yanga ni mabingwa watetezi wat aji hilo.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanaanza kazi kwenye mashindano hayo kwa kuendeleza pale ambapo waliishia msimu uliopita kwa kuwa walitwaa taji hilo.
“Tunakwenda kuanza kwa kishindo kwenye CRDB Federation Cup kwa kuangalia wapi ambapo tuliishia na kwa kuwa ni mabingwa watetezi tunakwenda kuanza kibingwa kwa kusaka ushindi kwa kishindo.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu kwa kuwa maandalizi yapo vizuri na kila kitu kinakwenda sawa ambacho tunahitaji ni ushindi kwenye mchezo wetu Jumamosi.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.