SIMBA TAMBO TUPU KISA MITAMBO HII YA MABAO

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wachezaji wao wanatimiza majukumu kwa umakini jambo ambalo linaongeza hatari kwao wakiwa mbele kwa kufunga mabao mengi kwenye mechi za ushindani.

Ipo wazi kwamba Leonel Ateba ni kiongozi kwenye safu ya ushambuliaji akiwa ametupia mabao matano na kinara wa kutengeneza pasi za mwisho ni kiungo mshambuliaji Jean Ahoua mwenye pasi tano za mabao.

Mbali na kutoa pasi Ahoua ni mkali kwenye kucheka na nyavu akiwa amefunga jumla ya mabao 7 yote akiwa ametumia mguu wa kulia kuwapa tabu wapinzani wake ndani ya ligi namba nne kwa ubora.

Ahmed Ally, Meneja Habari wa Simba amesema kuwa wachezaji wao wote wanafanya kazi kubwa kwa ushirikiano jambo ambalo linawapa matokeo mazuri.

“Unaona safu ya ushambuliaji ya Simba namna inavyofanya kazi ule mstari wa mbele una balaa zito kuna Ateba yupo na Ahoua ni balaa kwelikweli wanafanya kazi, yule Ateba ni mfungaji halafu Ahoua bado hajafikia asilimia 100.”

Januari 26 2025 Simba itakuwa kwenye kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Kilimanjaro Wonders SC ambao utachezwa Uwanja wa Manispaa ya KMC Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.