SIMBA HESABU KUBWA KWA WAPINZANI WAO ZIPO HIVI

SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wao dhidi ya Kilimanjaro Wonders hivyo wataingia kwa tahahari lengo ikiwa ni kupata matokeo mazuri.

Simba ikiwa imetoka kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Constantine, Uwanja wa Mkapa Januari 19 2025, itakuwa na kibarua kingine uwanjani kusaka ushindi Januari 26 2025 na huu ni mchezo wa mtoano atakayepoteza safari imemkuta.

Matola amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo hivyo wataingia uwanjani kwa hesabu za kupata ushindi licha ya kukutana na timu ambayo hawaijui namna ambavyo inacheza kwenye mechi za ushindani.

“Tunakwenda kucheza mchezo wetu  kama fainali kwa kuwa tunatambua ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi na malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda mchezo wetu muhimu.”

Mabingwa watetezi wa taji la CRDB Federation Cup ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu,Sead Ramovic mwenye tuzo ya kocha bora ndani ya ligi namba nne kwa ubora Desemba 2024.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.