ZIMBWE ANAANGUKA NA KUINUKA, SOMO TOSHA

LEGEND kwenye uandishi wa Habari za Michezo Bongo Saleh Ally, maarufu kama Jembe ameweka wazi kuwa beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr ni kipimo cha shida na raha kwenye soka kwa kuwa amekuwa akianguka na kuinuka kwenye upambanaji.

Ipo wazi kwamba Zimbwe ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids na amekuwa akifanya kazi yake kwa umakini akishirikiana na wachezaji wengine ndani ya uwanja.

Simba imetinga hatua ya robo fainali katika Kombe la Shirikisho wakiwa ni namba moja kwenye Kundi A baada ya kuvuna jumla ya pointi 13.

Jembe kuhusu Zimbwe ameandika namna hii:- “Zimbwe ni kipimo cha shida na raha katika soka… Lakini ni beki wa kushoto wa mguu wa kushoto ambaye ameandika rekodi kubwa katika suala la performance.

Kuna msimu mmoja, Zimbwe alicheza mechi zote 30 za ligi kwa dakika zote. Kaanguka mara kadhaa, mara zote ameinuka na kuwa bora. Hakatai wala hakasiriki kukosolewa. He is TOO POSITIVE…

Captain MITANO TENA