KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic kwenye gusa achia twende kwao balaa zito wakiituliza Simba mazima kwenye kasi ya utupiaji wa mabao ndani ya ligi namba nne kwa ubora.
Ikumbukwe kwamba Desemba 2024 ni Clement Mzize ambaye ni mshambuliaji alichaguliwa kuwa mchezaji bora na Sead alitangazwa kuwa kocha bora kutokana na ushindi mfululizo kwenye mechi nne ambazo Yanga ilicheza.
Rekodi zinaonyesha kuwa ni mabao 16 Yanga ilifunga kwenye mechi hizo nne huku safu ya ulinzi ikiruhusu mabao mawili yakufungwa iliuwa kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Mbali na kutupia mabao 16 kwenye mechi nne rekodi zionyesha kuwa Yanga ni namba moja kwa timu zilizofunga mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 32 baada ya kucheza mechi 15 za ligi mzunguko wa kwanza.
Mkali wa kucheka na nyavu ndani ya Yanga ni Mzize ambaye kafunga jumla ya mabao 6 na katoa pasi nne za mabao akihusika kwenye mabao 10 kati ya 32 ya timu hiyo iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Simba ni mabao 31 imefunga ndani ya ligi baada ya mechi 15 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi 40 huku Yanga ikiwa na pointi 39 nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.