MASTAA wawili ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ni balaa zito kwenye mapigo ya penalty kwa kuwa wakishika mpira tu lazima wafunge ikiwa watapewa jukumu la kazi hiyo.
Ikumbukwe kwamba kupiga penati kunahitaji umakini mkubwa kutokana na asilimia kubwa wengi kuhesabu kuwa ni bao lakini wapo mafundi wakubwa ambao hukosa penati.
Ipo wazi kwamba mkali wa kutuma mguu wa kushoto Bongo, Aziz Ki ni miongoni mwa nyota ambao kwa msimu wa 2024/25 alikosa penalty ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ukirudi kwa Ateba na Ahoua wamekuwa na nyota kali kwenye upande wa mapigo ya adhabu hizo ambapo wote kazi zao zote zilizama kwenye nyavu wakiwapa mateso makipa ndani ya uwanja.
Ateba katupia mabao matano kwenye ligi katika hayo ni mabao matatu kafunga kwa penati na mawili alikuwa kwenye mwendo ndani ya ligi. Yale yote ya penalty alipopewa alifunga.
Ahoua ni mabao 7 kafunga ambapo mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia akifunga yote kwa mguu huo ni mabao matatu kafunga kwa penati miongoni mwa timu alzifunga ni dhidi ya Dodoma Jiji na JKT Tanzania.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.