SIO kuongoza ligi tu ndani ya Bongo bali mpaka kwenye msimamo wa timu namba moja kwa kupata penalti nyingi ni namba moja Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Ikumbukwe kwamba penati ni adhabu ambayo huwa inatolewa kutokana na mchezaji wa timu moja kufanyiwa faulo ndani ya eneo la 18 na wakati mwingine mchezaji ambaye sio kipa wat imu husika kushika kwa makusudi mpira huo kwa lengo la kuokoa.
Tumeshuhudia penalti kadhaa ambazo Simba ilipata zikazua gumzo moja wapo ni ile dhidi ya Dodoma Jiji ambayo ilionekana kuwa na utata kutokana na beki wa Dodoma Jiji kuonekana kucheza mpira na sio mwili wa beki Mohamed Hussen ambaye alionekana kuanguka chini.
Ukiweka kando hiyo hata penalti ambayo Simba walipata dhidi ya JKT Tanzania iliyofungwa na Jean Ahoua Uwanja wa KMC, Complex ilileta utata kutokana na namna ambavyo Shomari Kapombe alianguka kwa kile kilichoelezwa kuwa ulikuwa ni mtego na mwisho mchezaji wa JKT Tanzania akajaa.
Yote kwa yote penalti ni faida kwa timu inayopata na ikifunga ni faida zaidi akikosa mfungaji heshima hurudi kwa kipa ambaye ataonekana kuwa ni shujaa kwenye mchezo husika.
Hapa tunakuletea timu ambazo zimepata penati nyingi mzunguko wa kwanza namna hii:-
Kwenye mabao 31 Simba ni mabao sita imefunga kwa penalty. Mastaa wawili ni vinara kwa utupiaji kwa mapigo ya penati wakiwa na rekodi ya kufunga zote ni Leonal Ateba ambaye ni mshambuliaji huyu kafunga penalti 3 sawa na Jean Ahoua.
Coastal Union ya Tanga imepata jumla ya penalty 5 ndani ya ligi ambapo timu hiyo msimu wa 2024/25 haijawa kwenye ubora wake iliomaliza nao msimu uliopita wa 2023/24.
Namungo FC ilipata penalty 5 pia huku nyota mwenye mabao mengi ya penalty akiwa ni kiraka Erasto Nyoni huyu katupia kambani penalty mbili mtaalamu huyu kwenye mapigo huru.
Tabora United ile iliyoitungua Yanga mabao 3-2 Uwanja wa Azam Complex ilipata jumla ya penalti 5 pia ikiwa kwenye orodha ya timu ambazo zimepata penalty nyingi.
Matajiri wa Dar, Azam FC ni penalty tatu walipata n azote walifunga kupitia kwa kiungo Feisal wa Azam FC ambaye jumla kafunga mabao manne na matatu ilikuwa kwa penati.
Yanga ni penati 3 imepata na zote mpigaji ni Aziz Ki alipata bahati ya kufunga mabao mawili kwa mapigo ya penati ndani ya Yanga na alikosa penalti moja ilikuwa dhidi ya Tabora United.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.