Droo ya kupanga makundi ya mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025) inatarajiwa kufanyika Januari 27, 2025, jijini Rabat, Morocco. Hafla hiyo itawakutanisha wawakilishi wa timu 24 zilizofuzu, zikiwemo zile kutoka Afrika Mashariki kama Tanzania.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026 ambapo waandaaji wa mashindano hayo ni Morocco.