MASHINE MPYA YANGA MOJA YAKWAMA NYINGINE FRESH

BEKI wa kupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Yanga, Israel Mwenda ruksa kuwavaa wapinzani wa timu hiyo MC Alger, Januari 18 2025 mchezo wa hatua ya makundi.

Ni mashine mbili za kazi zimetambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga kwenye dirisha dogo ambapo katika hao mmoja mambo fresh kimataifa na mwingine amekwama kuwa sehemu ya kikosi kwenye anga la kimataifa.

Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga ni kwamba tayari usajili wa Mwenda unekamilika na yupo huru kucheza mechi zote za ushindani ikiwa ni dhidi ya MC Alger, gusa achia twende robo fainali.

Nyota mwingine moya wa Yanga Jonathan Ikangalombo yeye hatacheza mechi za kimataifa kwa kuwa tayari alishacheza mashindano ya kimataifa kabla ya kutambulishwa Yanga.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema: “Mwenda ikiwa mwalimu ataona anafaa basi atamtumia, Jonathan hatakuwa kwenye mechi za kimataifa taratibu hazimruhusu kwa sababu mashindano haya hayamtaki mchezaji mmoja kucheza sehemu mbili mashindano haya.

“Ikangalombo yeye alicheza hatua ya awali akiwa na AS Vita hivyo katika mechi za kimataifa hatacheza, yeye ana kazi maalumu maana ni winga, “.

Januari 18 Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye kete ya mwisho wakiwa Uwanja wa Mkapa ili kutinga hatua ya robo fainali ni lazima kushinda mchezo huo na kufikisha pointi 10 kwa kuwa wapo nafasi ya tatu na wapinzani wao wapo nafasi ya pili na pointi 8.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.