SIMBA WANAPIGIA HESABU NAFASI HII ANGA LA KIMATAIFA

FADLU Davids, mpanga ramani wa kikosi cha Simba ambaye ni Kocha Mkuu amesema kuwa baada ya kufanikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, sasa hesabu ni kuona wanashinda mchezo ujao Uwanja wa Mkapa.

Simba imefikisha pointi 10 kwenye kundi A baada ya kucheza mechi 5 mchezo wake uliopita ilipata pointi moja kwa kufungana bao 1-1 dhidi ya Bravos.

Bao pekee la Simba lilifungwa na Leonel Ateba dakika ya 69 huku lile la Bravos likifungwa dakika ya 13 na Abdenego.

Fadlu amesema kuwa kutinga hatua yar obo fainali ilikuwa malengo yao na yametimia sasa kazi kubwa ni kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Constantine ambao utakuwa wa mwisho kwenye hatua ya makundi.

“Kutinga hatua ya makundi tumefanikiwa hilo ninawapongeza wachezaji na sasa malengo yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo kwenye mchezo wetu ujao ili kuona namna gani tunamaliza tukiwa tunaongoza kundi.”

Katika mchezo ujao wa Simba, unaotarajiwa kuchezwa Januari 19 2025 saa 10:00 jioni hakutakuwa na mashabiki baada ya Simba kupigwa rungu na CAF hivyo ni vita ya kuwania nafasi ya kwanza kimyakimya.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.