ALLY KAMWE ATANGAZA BOMU JIPYA YANGA – MC ALGERS WAMEKULA NYOYA – AFICHUA SIRI za NDANI za TIMU- VIDEO

Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe amefunguka na kueleza kuwa walitegemea wapinzani wao MC Alger walitarajiwa kufika asubuhi ila hawajafika.

“Hakuna kiumbe hai yeyote anayetudai Yanga tumelipa madeni wachezaji na makocha wanaotudai, tumefunguliwa kusajili” Ali Kamwe.

“Taarifa ambazo tunazo ni kuwa wapinzani wetu walipaswa kuingia nchini alfajiri ya kuamkia leo, lakini mpaka leo hatujawaona na sisi kama klabu tulifanya wajibu wetu lakini hawakutokea, tukipata taarifa rasmi basi tutawajuza. Kimsingi tunahitaji kuwaona uwanjani jumamosi mengine hayatuhusu.

Mechi mbili za awali hatukuwa na alama hata moja, lakini hivi sasa tunaongelea kushinda mchezo kwa idadi yoyote ili tuweze kufuzu hatua ya robo fainali. Lakini ukweli ni kwamba hii mechi sio rahisi ni mechi ngumu mno. Nafikiri mnaona wanavyofanya ujanja ujanja wanakuja kwa mafungu mafungu. Wamedhamiria kuja kupata alama. Kila mwana yanga anapaswa kujua kuna jukumu zito la kuujaza uwanja”

“Niwapongeze mashabiki na wanachama wa Yanga SC, tiketi nyingi tayari zimeisha kabla hata mkutano wa hamasa au klabu kutangaza rasmi uuzwaji wa tiketi, mwamko wa Wanayanga umekuwa mkubwa sana, wananchi wameingia wenyewe kwenye mfumo wa N-Card na kununua tiketi bila klabu kutangaza chochote. Wananchi wameonesha kwa vitendo kwa kiasi gani wanaitaka mechi, VIP A tayar zimeisha.

Jukumu la kuujaza Uwanja ni jukumu la kila mwana Yanga, tuna mashabiki zaidi ya milion 40 Tanzania, tunashindwa nini kupata mashabiki 60,000 kuujaza uwanja? Nimefurahi kuona baadhi matawi wakifanya dua kuiombea klabu yao kwa kwenda kufanya charity, hilo ni jambo la kheri lakini kimsingi ukiacha dua tunahitaji full House kwa Mkapa. Ambacho wewe mwana Yanga unaamini kuwa ukifanya timu yako inaishinda basi kakifanye” Ally Kamwe