SIMBA YAKUTANA NA RUNGU ZITO KUTOKA CAF

HABARI ambayo haitapokelewa kwa shangwe na mashabiki wa soka Bongo kutoka Ligi namba sita kwa ubora Afrika ni hii inayohusu Klabu ya Simba.

Taarifa rasmi kutoka Simba iliyotolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji wa Simba Zubeda Sakuru imeeleza kuwa timu hiyo imepokea maamuzi kutoka Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, (CAF) kuhusu vurugu zilizotokea kwenye mchezo dhidi ya SC Sfaxine Desemba 15 2024.

Uamuzi wa CAF umeifungia Simba mechi mbili ila adhabu imepunguzwa mpaka mechi moja kucheza bila mashabiki na faini ya Dola elfu 40,000.

Simba wameeleza kuwa bado wanaendelea kufanya utaratibu kushughulikia jambo hilo na kusitisha mauzo ya tiketi ya mchezo ujao dhidi ya Constantine unaotarajiwa kuchezwa Januari 19, Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.