MFUNGAJI Bora wa muda wote wa Timu ya taifa, Taifa Stars Mrisho Khalfan Ngassa yupo nchini Kenya ambaye yeye ni kati watu watakaochezesha droo ya upangaji wa Makundi ya michuano ya Chan mwaka 2024.
Kwa Mujibu wa Ngassa alipata mwaliko huo hivi karibuni kutoka Caf, ikimtaka kuwepo katika uchezeshaji wa droo hiyo itafanyika Kenya kesho Jumatano.
Ngassa ameungana na nyota wengine wa zamani wa Mataifa ya Kenya McDonald Mariga na nyota wa zamani wa Uganda Hassan Wasswa.
Huo ni mwaliko wa pili kwa kiungo huyo aliyecheza kwa muda mrefu na Klabu ya Yanga ambaye Januari 2024, Ngassa alipata mwaliko pia kutoka Caf kuhudhuria michuano ya Afcon 2023 iliyofanyika Ivory Coast.
Huu ni muendelezo wa CAF kutambua michango ya wachezaji wa zamani na kuwapa thamani ya kuwa sehemu ya shughuli mbalimbali za kisoka zinazoendelea kufanyika kwa maendeleo ya soka Afrika.