AZAM FC NA SAINI YA FEI TOTO WAZUA JAMBO

WAKATI kiungo Feisal Salum maarufu kama Fei Toto akiwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba na Yanga, uongozi wa Azam FC umezua jambo kimtindo kuhusu usajili wa nyota huyo.

Ipo wazi kwamba Feisal ni namba moja kwa watengeneza pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inadhaminiwa na NBC ikiwa ni ligi namba sita kwa ubora.

Fei katoa jumla ya pasi 9 za mabao na katupia mabao manne kambani katika mabao hayo manne ni matatu alifunga kwa penalti kiungo huyo ambaye mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.

Kupitia kwenye ukurasa wa Instagram, Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe ameuliza swali lenye mtego kwa timu ambazo zilikuwa zinatajwa kufika Azam Complex kuhitaji huduma za baadhi ya wachezaji.

“Mliosema mnakuja tuongee bado siku moja boss anawasubiri huku.”

Inatajwa kuwa hakuna timu ambayo imepeleka ofa ya kuhitaji saini ya nyota yoyote kutoka ndani ya Azam FC kwa wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.