WINGA DIALLO AONGEZA MKATABA MPYA MAN UTD HADI 2030

Winga Amad Diallo (22) raia wa Ivory Coast amesaini nyongeza ya mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Manchester United hadi Juni 2030.

“Nimekuwa na nyakati za ajabu na Man United tayari, lakini kuna mengi zaidi yanayokuja. Nina malengo makubwa katika mchezo huu.” ——imesema Amad ‘Ivorian Messi’ kama wanavyomuita baada ya kusaini mkataba huo.