SINGIDA BLACK STARS KWENYE VITA KUMUWANIA KIPA SIMBA

INATAJWA kuwa mabosi wa Singida Black Stars wapo kwenye vita ya kuwania saini ya kipa wa Simba Aishi Manula ambaye anatajwa kuwa kwenye rada za Azam FC pia.

ipa huyo msimu wa 2024/25 hajacheza mchezo wowote ndani ya Ligi Kuu Bara na namba moja ni Mousa Camara ambaye amekaa langoni kwenye mechi zote 15 za ligi.

Hayupo kwenye msafara uliopo Angola kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos unaotarajiwa kuchezwa Januari 12 2025 ikiwa ni hatua ya makundi.

Taarifa zinaeleza kuwa Singida Black Stars wanahitaji saini ya Manula kumuongezea ushindani kipa namba moja wa timu hiyo Metacha Mnata ambaye ni chaguo la kwanza katika timu hiyo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.