MWENYEKITI wa Simba, Murtanza Mangungu amesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa ni kupata matokeo kwenye mechi zijazo hivyo masuala ya kufikiria nani atapata nini kwa sasa iwekwe kando na badala yake nguvu iwe kwenye kupata ushindi.
Ikumbukwe kwamba Simba ipo kwenye kundi ambalo lina ushindani mkubwa kwa timu tatu kuwa kwenye ubora katika mechi za kimataifa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Licha ya Simba kuvuna pointi tisa ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi wakiwa nafasi ya pili vinara ni Costantine wenye pointi tisa mchezo ujao ni dhidi ya Bravos nafasi ya tatu na pointi 6.
Bravos ilipoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-0 Bravos bao la Jean Ahoua ambaye kwenye anga la kimataifa katupia mabao mawili na pasi mbili za mabao.
Mangungu amesema kuwa suala la kusema ni muda wa kutembea na calculator kwa sasa hilo inabidi liachwe na badala yake nguvu kubwa iwe kwenye kutafuta matokeo kwenye mech izote zilizobaki.
“Kikubwa tumetoka kupata matokeo kwenye mchezo wetu uliopita ugenini na sasa mpango mkubwa ni kuona kwamba tunakwenda kupata matokeo ugenini,hilo ni jambo la msingi kuliko kuanza kufikiria sualala kutembea na calculator kwa sasa.
“Pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wanapambana na kupata matokeo mazuri hili ni jambo la kujivunia na benchi la ufundi linastahili pongezi kutokana na kazi kubwa ambalo linaifanya.”
Mchezo ujao kwa Simba dhidi ya Bravos unatarajiwa kuchezwa nchini Angola, Januari 12 2025 saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.