WAKIWA kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Hilal unaotarajiwa kuchezwa Jumapili ya Januari 12 2025 nchini Mauritania Yanga kutoka Tanzania itawakosa wachezaji watatu kwenye uwanja kwa kuwa hawapo kwenye mpango wa benchi la ufundi.
Ni Uwanja wa de la Capitale watashuka Yanga chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic kusaka pointi tatu muhimu wakiwa na kumbukumbu yakupoteza mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Yanga 0-2 Al Hilal.
Al Hilal tayari imeshakata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na pointi 10 katika kundi A inakutana na Yanga yenye pointi nne ikiwa nafasi ya tatu.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa maandalizi yapo vizuri kuelekea mchezo huo ambapo wapo wachezaji ambao hawatakuwa kwenye mpango wa mchezo wao ujao kutokana na sababu malumu.
“Kuna wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa bado hawajawa fiti ambapo ni Aziz Andambwile, Yao na Maxi hawa bado hawajaimarika na ushauri wa madaktari ni kwamba waendelee kuwa chini ya uangalizi maalumu.
“Lakini Clatous Chama yeye yupo tayari na ameanza mazoezi na wachezaji wenzake atakuwa sehemu ya msafara kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Al Hilal.”
Tayari kikosi cha Yanga kimeanza safari kuwakabili wapinzani wao ambapo hesabu kubwa ni kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.