“Kwenye mechi zetu mbili tulizocheza Uwanja wa Mkapa mashabiki hawakujitokeza kwa wingi hivyo kuelekea mchezo wetu wa funga kazi dhidi ya Costantine wajitokeze kwa wingi na tunahitaji kuona Uwanja wa Mkapa unajaa.”
Ni maneno ya Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ikiwa ni kazi maalumu kwa mashabiki wa timu hiyo inayopeperusha bendera kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya makundi.
Mchezo ujao kwa Simba iliyo kundi A inatarajiwa kumenyana na Bravos Januari 12 tayari kikosi kimewasili Dar baada ya kuwa na mchezo dhidi ya SC Sfaxine ya Tunisia wakivuna pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Jean Ahoua.
Ally amesema: “Mechi zetu zote mbili zilizobaki ni muhimu na kikubwa ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri, wachezaji wanajituma na mashabiki wanaoaswa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu wa funga kazi Uwanja wa Mkapa.”
Mchezo ujao kwa Simba itakuwa ugenini dhidi ya Bravos ambapo walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-0 Bravos, bao la kiungo Jean Ahoua kwa mkwaju wa penalti. Mchezo ujao ni Januari 12 2025 itakuwa saa 1:00 usiku.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.