UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa ushindi mbele ya SC Sfaxinekwenye mchezo wa kimataifa uliochezwa nchini Tunisia sio mwisho wa mapambano kazi bado inaendelea katika mechi zijazo kimataifa.
Kwenye mchezo huo Januri 5 2025 Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo mtupiaji akiwa ni kiungo mshambuliaji Jean Ahoua dakika ya 34 tayari msafara wa wachezaji na viongozi wa Simba upo Dar kwa hesabu za maandalizi ya mchezo ujao watakaokuwa ugenini nchini Angola.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanashangilia ushindi lakini kwa kiwango kwa kuwa bado kazi haijaisha kutokana na kuwa na mechi nyingine mbele ngumu zaidi na kinachohitajika ni matokeo chanya.
“Baada ya kumaliza mchezo wetu ugenini na kupata pointi tatu muhimu tunapaswa kufurahi lakini kwa kiwango kwa kuwa bado tuna kazi nyingine ya kufanya hilo lipo wazi. Tutakuwa na mchezo Januari 9 Angola baada ya kumaliza mchezo huo tutakuwa na mchezo nyumbani.
“Mechi yetu dhidi ya Bravos mashabiki walikuja wachache, mechi yetu ya pili dhidi ya SC Sfaxine mashabiki walikuja wachache sasa kwenye mechi yetu ya mwisho funga kazi dhidi ya Costantine tunahitaji mashabiki waujaze Uwanja wa Mkapa.”
Ikumbukwe kwamba Januari 9 Simba itakuwa ugenini kusaka pointi tatu dhidi ya Bravos na walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-0 Bravos kwa bao la Ahoua ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.