MZIZE KWENYE HESABU KUBWA KIMATAIFA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize amesema kuwa furaha kubwa ni kuona wanaendelea kuwa kwenye mwendelezo wa kupata matokeo kwenye mechi za kimataifa ili kufanikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ikiwa Uwanja wa Mkapa iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 TP Mazembe huku kamba mbili zikifungwa na Mzize na bao moja lilifungwa na Aziz Ki ilikuwa ni Januari 4 2025.

Mzize amesema kuwa walikuwa wanahitaji kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya TP Mazembe jambo ambalo liliwezekana licha ya ushindani kuwa mkubwa kwenye mchezo huo.

“Ilikuwa ni muhimu kwetu kupata matokeo mazuri licha ya ushindani ambao ulikwepo kwa hatua hii tunaamini kwamba tutazidi kupambana kwa mechi zijazo ili kufanikisha malengo ya kutinga hatua ya makundi.”

Kwenye Kundi A la Yanga ni Al Hilal hawa wametinga hatua ya robo fainali wakiwa na pointi 10 nafasi ya kwanza huku MC Alger ni nafasi ya pili pointi 5, Yanga nafasi ya tatu pointi nne na TP Mazembe nafasi ya nne pointi mbili.

Timu tatu bado safari mbichi kutokana na kila timu kuwa na nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali hivyo ili Yanga kutoka Tanzania kufanikisha malengo hayo ni lazima kushinda mechi zake.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.