MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamerejea mazoezini ndani ya mwaka mpya 2025 kuendeleza ushindani katika mechi zijazo kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba sita kwa ubora Afrika.
Mchezo wa funga kazi 2024 kwa Azam FC ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa Desemba 27 2024 na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 3-1 JKT Tanzania.
Idd Nado katika mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora alifunga mabao mawili akitumia pasi za Feisal Salum ambaye anafikisha pasi tisa za mabao.
Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 vinara ni Simba wenye pointi 40 baada ya kucheza mechi 15 nafasi ya pili Yanga wenye pointi 39 baada ya kucheza mechi 15.
Fei amekuwa kwenye mwendelezo wa ubora wake ndani ya uwanja katika mechi za ligi msimu wa 2024/25 akisaka rekodi yake ya msimu uliopita mabao 19 na pasi 7 ambapo kwa sasa kafunga mabao manne akihusika kwenye mabao 13 kati ya 25 yaliyofungwa na timu hiyo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.