RAIS SAMIA AIPONGEZA KLABU YA SIMBA SC BAADA YA USHINDI DHIDI YA CS SFAXIEN

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Simba SC baada ya ushindi dhidi ya CS Sfaxien.

Kupitia mtandao wake wa kijamii ameandika-:
“Hongera kwa Klabu ya Simba kwa ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) dhidi ya CS Sfaxien”

“Mmewapa mashabiki na Watanzania wote kwa ujumla burudani na furaha. Endeleeni kuweka juhudi na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu kimataifa, mkitumia mazingira bora ya kufanya vyema kwenye michezo tunayoendelea kuyaboresha siku baada ya siku”

“Ninawatakia kila la kheri katika michezo iliyosalia” ameandika Rais Samia