GUSA achia twende kwao ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic ina balaa zito baada ya pointi tatu kubaki Uwanja wa Mkapa huku mshambuliaji Clement Mzize akifunga moja ya bao kali ambalo limeandika rekodi yake kwa msimu wa 2024/25.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Januari 4 2025 Yanga walianza kufungwa ila wakaweka usawa kupitia kwa Mzize akitumia pasi ya Boka aliyesababisha penalti katika harakati za kuokoa hatari kuelekea kwa Djigui Diarra.
Mzize ambaye alikuwa ni nyota wa mchezo alitupia mabao mawili dakika ya 33 na 60 na bao moja lilifungwa na Stephan Azizi Ki dakika ya 56.
Bao pekee la TP Mazembe lilifungwa na Alioune Faty dakika ya 16 kwa mkwaju wa penalti iliyomshinda Djigui Diarra.
Yanga inafikisha pointi nne katika hatua ya makundi baada ya kucheza mechi nne ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na TP Mazembe inabaki na pointi mbili nafasi ya nne hivyo kete zake mbili inasaka pointi sita kutinga hatua ya robo fainali.