MAMELODI YAKUBALI KICHAPO LIGI YA MABINGWA

Mamelodi Sundowns imekubali kichapo cha 1-0 dhidi ya wenyeji, Raja Casablanca kwenye mchezo wa raundi ya nne wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika dimba la Larbi Zaouli.

FT: Raja AC 🇲🇦 1-0 🇿🇦 Mamelodi Sundowns
⚽ 45+2’ Benamar

Timu zote zimemaliza mchezo zikiwa pungufu wachezaji wawili wa Mamelodi Sundowns wakioneshwa kadi nyekundu huku mchezaji mmoja wa Raja AC akioneshwa kadi nyekundu.

FT: AS FAR Rabat 🇲🇦 2-0 🇨🇩 Maniema
⚽ 12’ Ouarkhane
⚽ 45+3’ Zouhzouh

MSIMAMO KUNDI B
1. 🇲🇦 AS Far Rabat— mechi 4—pointi 8
2. 🇿🇦 Mamelodi— mechi 4—pointi 5
3. 🇲🇦 Raja AC CR — mechi 4—pointi 4
4. 🇨🇩 Maniema — mechi 4—pointi 3