YANGA SIO KINYONGE KUWAKABILI TP MAZEMBE

KUTOKA ligi namba 6 kwa ubora Afrika, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa taji la ligi msimu wa 2024/25 wamebainisha kwamba wapo tayari kusaka pointi tatu mbele ya wapinzani wao TP Mazembe ambao tayari wameshatua ardhi ya Tanzania ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo uliopita wa makundi wakiwa ugenini dhidi ya TP Mazembe, Yanga iliambulia pointi moja kwa sare ya kufungana bao 1-1 ikipata pointi kwa mara ya kwanza kwenye hatua za makundi kwa kuwa kwenye mechi zake mbili kimataifa ilipoteza.

Januari 4 2025 Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic itakuwa Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya TP Mazembe ambao nao wanazihitaji kwa udi na uvumba ndani ya uwanja.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amebainisha kuwa tayari kikosi hicho kipo kwenye mwendo mzuri jambo ambalo linawapa nafasi ya kupata matokeo chanya mbele ya TP Mazembe na hesabu kubwa ni kupata pointi tatu muhimu.

“Tutakuwa nyumbani kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya TP Mazembe kikubwa ni kuona tunapata pointi tatu kwani tutakuwa nyumbani na wachezaji wanatambua kwamba huu ni mchezo muhimu nasi tutapambana kwa ajili ya kuona kwamba tunapata matokeo mashabik wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwapa nguvu wachezaji.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.