MWAMBA FEI TOTO NGOMA NZITO KUSEPA AZAM FC

NGOMA ni nzito kwa nyota wa Azam FC, Feisal Salum kusepa hapo kutokana na dau ambalo linahitajika kuwa zaidi ya milioni 500 kuvunja mkataba wake.

Inatajwa kuwa matajiri kutoka Kariakoo ambao ni Simba na Yanga wapo kwenye rada za kuinasa saini ya kiungo huyo ambaye ni namba moja kwa pasi za mwisho Bongo.

Ametoa pasi tisa za mabao na kufunga mabao manne hivyo kahusika kwenye mabao 13 kati ya 25 yaliyofungwa na timu hiyo baada ya kucheza mechi 16 msimu wa 2024/25.

Taarifa zinaeleza kuwa timu ambayo ilikuwa ikimtazama kwa ukaribu Fei Toto ni Simba na ilikuwa tayari kuipata saini yake lakini dau lake kuwa kubwa ni kipengele kwa mabosi hao kuweka mkwanja mrefu kwa kuwa ni dirisha dogo.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa kuna ugumu mkubwa kwenye kipindi cha dirisha dogo kupata wachezaji wazuri kwa kuwa wanakuwa na mikataba katika timu zao ambazo nazo zinakuwa zinahitaji huduma za wachezaji hao.

“Kwenye dirisha dogo la usajili huwa kunakuwa na mengi yanatokea hasa kipindi cha dirisha dogo kuna kazi kubwa kuwapata wachezaji wazuri kwa kuwa wengi huwa wanakuwa na mikataba na timu zao huwa zinawahitaji, kikubwa ni kuwa na subira mambo mazuri yanakuja.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.