HII HAPA RATIBA YA YANGA KIMATAIFA

KUTOKA Ligi Kuu Bara namba 6 kwa ubora Afrika, Yanga inaoeperusha bendera katika Ligi ya Mabingwa Afrika na itakuwa na kete 3 2025 kusaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Ni Januari 4 2025 dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni katika mchezo uliopita walipokutana Yanga iligawana pointi moja na miamba hawa kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Januari 15 2025 itakuwa dhidi ya Al Hilal ambapo Yanga watakuwa ugenini nchini Mauritania ngoma inatarajiwa kupigwa saa 4:00 usiku katika mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

Yanga v MC Alger hii itapigwa Uwanja wa Mkapa Januari 18 2025 saa 10:00 jioni, kwenye mchezo waliokutana ugenini Yanga ilipoteza pointi tatu muhimu.

Kete mbili za Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic itakuwa nyumbani na kete moja itakuwa ugenini.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.