WAWAKILISHI wa Tanzania katika anga la kimataifa Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika wanakete zao kusaka pointi tatu muhimu.
Simba kutoka ligi namba sita kwa ubora Afrika katika Ligi Kuu Bara wanaongoza wakiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 15.
Januari 5 itakuwa SC Sfaxine v Simba, ngoma itapigwa saa 1:00 usiku itakuwa 2025, Tunisia katika mchezo waliocheza Uwanja wa Mkapa Simba ilikomba pointi tatu kwa ushindi wa bao 2-1.
Bravos v Simba, Januari 12 2025 itakuwa Angola saa 1:00 usiku walipokutana Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-0 Bravos kwa bao la Jean Ahoua.
Simba v Constantine Januari 19 2025 Uwanja wa Mkapa muda utapangwaambapo ugenini Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.
Katika mechi tatu Simba itacheza mbili ugenini na moja nyumbani katika msako wa pointi tisa katika anga la kimataifa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.