KWENYE mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Singida Black Stars dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Liti, rekodi zinaonyesha kuwa dakika ambazo mpira ulichezwa hazikugotea 90 bali zilikuwa ni 72.
Sababu kubwa iliyofanya dakika 90 zisiwe kwenye mchezo mazima ni kutokana na upotevu wa muda hasa katika dakika 45 za mwanzo wachezaji wa Singida Black Stars kabla ya kufungwa bao dakika ya 42 walikuwa wakitumia sekunde zaidi ya 10 kwenye kila tukio.
Ikiwa ni tukio la kurusha watayeyusha sekunde zaidi ya 10 na ikiwa ni goal kick mlinda mlango Metacha Mnata atavuta mpaka sekunde 30 ila walipofungwa waliongeza hali ya kuwa kwenye haraka.
Kipindi cha pili ilikuwa ni kwa upande wa Simba ambao walikuwa wakivuta mpaka sekunde 10 kwenye mapigo ya faulo na Mousa Camara naye aliingia kwenye mtego wa kupoteza muda.
Dakika moja iliyeyuka kwa wachezaji wa Simba kushangilia bao ambalo walifunga dakika ya 42 kupitia kwa Fabrince Ngoma kwa kona iliyopigwa na Jean Ahoua.
Mchezaji ambaye alikutwa kwenye mtego wa kuotea mara nyingi zaidi alikuwa ni Elvis Rupia wa Singida Black Stars na miongoni mwa dakika ambazo alikuwa kwenye mtego wa kuotea ilikuwa dakika ya 45, 68, 72.
Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Liti, Desemba 28 2024 na mwamuzi wa kati alikuwa ni Shomari Lawi, ulikuwa mubasahara Azam TV.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.