HAWA HAPA NI NAMBA MOJA KWENYE LIGI BORA AFRIKA

KWENYE ligi namba sita kwa ubora Afrika, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ni namba moja kwa pasi za mwisho akiwa nazo 9 na katupia mabao manne.

Ipo wazi kuwa Azam FC wnatumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za nyumbani wamekuwa kwenye ubora wao katika mechi za hivi karibuni na walipokamilisha mechi 15 walikuwa namba moja kwenye msimamo.

Mchezo wao wa Desemba 27 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 3-1 JKT Tanzania, mabao ya Pascal Msindo na Idd Nado ambaye alifunga mawili akitumia pasi za Fei ambaye ni namba moja kwa wakali wa kutengeneza pasi za mwisho.

Elvis Rupia ni namba moja kwenye utupiaji  mabao akiwa katupia mabao 8 ndani ya msimu wa 2024/25 yeye yupo ndani ya kikosi cha Singida Black Stars.

Katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Desemba 28 2024 Rupia alianza kikosi cha kwanza alikwama kufunga kwenye mchezo huo ambao baada ya dakika 90 ubao ulisoma Singida Black Stars 0-1 Simba bao la Fabrince Ngoma.

Kwenye upande wa mabeki namba moja kwa kucheka na nyavu ni Ibrahim Bacca mwenye mabao manne ambapo katika hayo moja alifunga kwa pigo la mkono ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Makipa nao wapo kazini ambapo kipa wa Simba, Mousa Camara ni namba moja kwa makipa ambao wametoka na hati safi nyingi katika mechi za lig.

Ni mechi 15 amekaa langoni Camara akiwa hajafungwa kwenye mechi 12 msimu wa 2024/25 yeye akiwa ni kipa aliyecheza mechi zote za mzunguko wa kwanza.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.