WATU 124 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA NDEGE KOREA KUSINI

Watu takriban 124 kati ya 181 hadi sasa wamethibitika kufariki dunia baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata ajali na kudondoka wakati inatua katika uwanja wa ndege wa Muan nchini Korea Kusini ilipokuwa ikitokea Bangkok, Thailand.

Video mbalimbali mtandaoni zinaonesha ajali hiyo ya ndege aina ya Boeing 737-800 inayosimamiwa na Shirika la ndege la Jeju Air, ikitoka kwenye njia ya kurukia na kuangukia ukuta, kabla ya kuanza kuwaka moto.

Hadi sasa hakijapatikana chanzo cha ajali hiyo japokuwa Idara ya zima moto ya uwanja huo wa ndege imesema huenda wanyama kama ndege walisababisha hitilafu kwenye ndege hiyo au hali mbaya ya hewa pia inaweza kuwa chanzo, hata hivyo uchunguzi bado unaendelea.

Kati ya walionusurika kifo, wawili ni wafanyakazi wa ndege hiyo.

Chanzo:BBC